
SARATANI NI NINI?
Saratani ni jina la gonjwa ambao hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
NINI KINATOKEA
Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takriban miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake.
Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine.
Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini humo, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.
VIHATARISHI VINAVYOCHANGIA SARATANI YA TEZI DUME
· Umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
· Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
· Suala jingie ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
· Vilevile wataalamu wanatuambia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
· Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.
Tunataka kujua ni hospitali zipi wanatoa huduma za upimaji Tanzania nasi wenye vipato vidogo tuwapeleke baba zetu. Ni muhimu tafadhari!
ReplyDeleteNi vizuri kujua ilikuweza kujipanga ukijikuta na matatizo kama hayo.
ReplyDeleteThis is a very good article, well researched. Prosteta cancer kills a lot of people.if It is not diagnose early it will spreed to other organs. Yearly check up very important. Eating healthy food and exercise. Good Health is the best thing you can give to your self
ReplyDeleteDown memory lane.
ReplyDeleteMiaka mingi sana iliyopita tulipokuwa Tabora Boys, mimi na jamaa mmoja aitwaye Charles Shasha tulichukuliwa na mwalimu wetu Mr Gray na tukaenda Tabora Govt hospital kuangalia operesheni,Tuliingizwa theatre na tukaona what I now know to be an open prostatectomy.
Samahani, jamaa kaniuliza what are you talking about in your down memmory lane.What I am trying to say is that the type of surgery is performed in Bongo, I personally witnessed one being done more that 40 years ago.
ReplyDelete