Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo kuhusu masuala
ya haki za binadamu wakifuatilia hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. George Masaju (hayupo pichani) iliyotolewa leo Kunduchi
Beach Resort. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Taasisi za Kitaifa
za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya
mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg
(RWI) ya Sweden na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG)
kwa ufadhili wa SIDA.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba
yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu
kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi
za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba
yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu
kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi
za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo ya masuala ya haki za
binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. George Masaju
(waliokaa, wa pili kutoka kushoto) muda mfupi baada ya kufungua rasmi
warsha hiyo Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akibadilishana
mawazo na Mwakilishi wa Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na
Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden, Ms. Janne Holck
Clausen (katikati) na Mratibu wa Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki
za Binadamu Afrika (NANHRI), Ms. Flavia Mwangovya muda mfupi baada ya
ufunguzi rasmi wa warsha ya mafunzo ya siku tano kwa taasisi za
kitaifa za haki za binadamu Afrika huko Kunduchi Beach Resort leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...