Tafrani kubwa imezuka jioni ya leo wakati wa Mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere wa kujadili umuhimu wa kuzingatia Mambo ya msingi katika katiba inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliokuwa ukifanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.

Chanzo cha Tafrani hiyo, inaelezwa kuwa wakati Jaji Warioba akiongea, baadhi ya watu waliokuwepo kwenye mdahalo huo  walisimama na kuinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya rasmu ya katiba ambayo wao wameshaikubali?

Likaanza zogo ambapo watu wengine walijaribu kuwanyang'anya yale mabango na kuyachana na wao wenye mabango kujihami. Ndipo vurugu/kashfa/matusi vikaanza kutolewa. Hali hii ilisababisha kushikana mnashati, kusukumana na kurushiana viti. 

 Mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa, ulirushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kwa kile kilichoelezwa kuwa maudhui ya kimtazamo uliolenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Tume ya Warioba na ile ya Bunge Maalum la Katiba. 
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya kuzuka kwa tafrani hiyo.
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na Wanausalama  kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya mambo kuharibika kutokana vurugu kubwa.
Ilikuwa ni mshikemshike na tafrani tupu.
Mdahalo ukiwa umesitishwa kwa vurugu hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Maumivu ya kichwa huanza polepole

    ReplyDelete
  2. yaani kum "manhandle" mtu mzima ni aibu kubwa

    ReplyDelete
  3. Next ni vita Tanzania. Naona hata hatuwezi kujadili mambo kwa amani.

    ReplyDelete
  4. Hawana kazi wauza maandazi

    ReplyDelete
  5. SITAELEWA KAMA HAKUNA MTU ALIYE KAMATWA KATIKA VURUGU HIZO KAMA KIONGOZI WA VURUGU.

    ReplyDelete
  6. Huyu mzee warioba nae hatulii nyumbani kutwa kuangaika angaika tuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna unalo lijua kuhusu nchi yako..wala maisha ya watoto wako baadae..ndio maana una muona Warioba hatulii..utaelewa baadae wakati hutaweza kusomesha wanao..au watoto wako wakishindwa kukusaidia hapo baadae..THINK BIG

      Delete
  7. Wewe Anon kwani kuna shida watu wakijadili mambo ya katiba. Unaona shida sana Jaji Warioba akiwa kwenye mdahalo? Huna aibu, kwanini atulie nyumbani? Kwa taarifa yako wala hahangaiki bali anatimiza wajibu wake. Mbona humzungumzii Makonda aliyeanzisha fujo na watu wake. Tuheshimu mawazo ya wengine pia....tushindane kwa hoja si kwa fujo, uwe na busara ndugu yangu.

    ReplyDelete
  8. The youth of Tanzania Universities. Enzi zetu tulikuwa tunaandamana kuping akina Kissinger na mishahara mikubwa ya wabunge etc. Hao vijana ndiyo maana hawajui hata kuuandiaka. It would be interesting to read their assignements. Sisi tulikuwa tunaheshimu wazee.

    Hivi polisi watachukua hatua gani? This would be very interesting.

    ReplyDelete
  9. Who is paying these hooligans? Police should lock them up. I can't wait to see what they will do to these stupid bouz.

    ReplyDelete
  10. Walipangwa ili wafikishe ujumbe au wampinge

    ReplyDelete
  11. It is shame

    ReplyDelete
  12. LETS BE REALLISTIC.
    kwani warioba wakati anafanya kazi yake ya kukusanya na kuratibu maoni kupitia tume ya mabadiliko ya katiba NI NANI ALIKUWA ANAMSIMAMIA NA KUMFUATAFUATA?? iweje leo yeye na tume yake wageuke kuwa VIRANJA wa BMK kiasi cha kutangaza mapambano ya wazi kiasi hiki?? nadhani huyu mzee kuna jambo analitafuta na sijui kama WAFADHILI wake wanajulikana

    ReplyDelete
  13. wewe anonymous usimkemee mzee warioba kuwa hatulii nyumbani,anajaribu kutuelewesha kile tunachohitaji watanzania.wewe kama umetumwa kama Makonda kaa kimya.Kwani kujadili jambo la msingi ni dhambi?au na wewe ni mkora kama Makonda?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...