Chumba cha Globu ya Jamii Kimepokea picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi,Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wa Globu ya Jamii alietuletea taswira hizi kuhusiana na hali ya barabara hiyo.
''Kama una safari ya kwenda Iringa-Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi basi sitisha safari kwani njia inefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado inawaka na inesambaa sehemu kubwa''
Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo la ajali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...