Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery 'Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Mac Reagan 'Kipara' na Mjuni Silvery 'Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Je! Sisi wanachama vipi hatukopeshwi?

    ReplyDelete
  2. Yaani sisi wanachama mbona hatushirikishwi kwenye Neema kama izo

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu hapo juu, walikuja wawakilishi wao kazini kwetu nikawauliza swali hilo wakanijibu pumba eti niombe. Mimi hoja yangu ilikuwa kupangisha wanasiasa nyumba zao hapa mjini hasa tabata wakati sisi wachangiaji tukikaa mbali Kibaha, Vikindu, Mkuranga n.k na hivyo kupunguza ufanisi kazini na kupelekea kutoongeza mapato.
    Pia wamejenga nyumba Pemba ambao hawachangii hata senti moja wakati kuna wahitaji wengi pande hii. We acha tu!

    ReplyDelete
  4. Mdau mwenzangu isome vizuri hiyo habari!
    MKoPO UTALIPWA KWA KIPINDI CHA MIAKA 15 maana yake wameuziwa kwa mortgage kama taratibu za NSSF zisemazo kuwa unalipia kidogo kidogo kila mwezi kwa miaka 15. Mimi binafsi nimechukua moja miezi 2 iliyopita. Nakushauri uende zilipo nyumba hizo Kijichi uonane na NSSF wana ofisi yao pale na utauziwa. Jamaa wako mahiri kweli na zoezi halichukui muda. Hakuna kona kona wala mazingira ya rushwa. Nawapongeza!
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  5. Anonymous # 4 tafadhali tupe ufahamu walau kiasi gani nyumba inagharimu au kwa mwezi makato ni kiasi gani ili uweze lipia hiyo miaka 15!
    Shukrani!

    ReplyDelete
  6. nyumba nzuri lakini barabara je mbona hazijamalizwa?

    ReplyDelete
  7. Wadau, mimi nilikuja Dar mwezi Julai nikanunua. Bei zatofautiana, ukenda watakuonesha. Kuna ramani ya kitongoji kizima cha NSSF Kijichi pamoja na orodha ya bei. Ukinunua cash bei inakuwa kama ilivyo kwenye karatasi ila kwa mortgage inaongezeka. And that's obvious, huku magharibi mambo ni hivo hivo, yaani kama una cash utapata nafuu. Mfano kuna za milioni 80, 90, 100 na zaidi. Pia kuna vitu kama VAT na kodi zingine on top.
    Sasa wewe mwenyewe utatazama upejipangaje. Mimi nimeamua kuchukua kwa kulipa kidogo kidogo, zaidi kidogo ya laki moja kila mwezi kwa miaka 15. Option ingine ni kukopa benki. Mfano CRDB wanatoa mikopo ambapo unapata pesa zote za kununua kisha unawalipa wao. so wewe angalia wapi ni nafuu, mortgage au mkopo benki.
    Uzuri ni kwamba tofauti na huku magharibi mortgage ni fixed kwa miaka yote.
    Unatakiwa kulipa kodi ya miezi 3 hapo hapo unapewa nyumba. Nenda kaonane nao kwa faida zaidi.
    ila uwe serious na umejipanga. Otherwise utaishia kulalama kama wengine kuwa nyumba hazinunuliki. Mimi na wenzangu wengi tu tumenunua. Nadhani nimesaidia kujibu swali lako mdau mwenzangu.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  8. wewe upo UK umekujaje kununua huku na sio mwanachama wa NSSF?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...