Kwa hisani ya Global TV online

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Makonda nimeshamsikia, ningependa sasa nimsikie Mzee Warioba mwenyewe anasemaje kuhusu kile kinachosemekana kwamba alivamiwa na Makonda. Ndugu zangu ni bora tukajaribu kusikiliza pande zote(haswa sisi ambao hatukuwepo ukumbini) kama ya kutoa hisia zozote kuhusu tukio hili la aibu.

    ReplyDelete
  2. Mtoa mada wa kwanza utasubiri sana tu....haukua mkutano wa watu wawili kama ambavyo maoni yako yana akisi uelewa hasa kuhusu kilichotokea.....

    ReplyDelete
  3. makosa yalikuwa ni kuruhusu wenye MABANGO kuingia nayo katika ukumbi wa mdahalo.wenye mabango wangeelekezwa mahali pa kusimama nje ya ukumbi kuonyesha ujumbe katika mabango yao.ndani ya ukumbi wa mdahalo hakutakiwa vurugu wala mabishano, kuzungumza ni kwa ruksa ya MODERATOR, na vilevile haitakiwi kushangilia, kupiga makofi, au vigelegele.

    ReplyDelete

  4. Ndugu zangu tunapokwenda si kwe mema tunapoongelea jambo la katiba si jambo la kuchezea katiba ni sheria ya nchi si ya chama na wala si ya mtu bali ni ya nchi katiba ni Mama na Baba wa sheria katika kuifanya nchi iendelehe au kuirudisha nyuma ,kwa nchi kuendelea ni lazima iwe na katiba ya ukweli ya haki katiba ya watu wote si ya vyama,katiba inayozifanya taasisi za serikali kufanya kazi kwa haki bila kuingiliwa katiba inayowafanya wananchi wote wa chini na wa juu kufata sheria zauwajibikaji kutoka chini mpaka chini.
    Ndugu zangu Babu yangu alisema muafrica ukimpa uhuru mwingi anajisahu na mwisho ndiyo haya tunayoyaona katika Tanzania ya leo wakati wa Mwalimu Tanzania ilikuwa na amani Tanzania ilikuwa na heshima Tanzania ilipita katika mithihani mizito sana wakati huo dunia iliuwa na sehemu mbili upande wa East na upande wa West ,ilipita kwenye kipindi cha njaa mpaka tukala ugali wa majano ,vita ya kagera na mpaka mwalimu alipotoka madarakani kwa upande wangu pamaoja na kuwa mwalimu akuweza kutuweka pazuri katika swala la uchumi lakini aliacha nchi yenye amani,umoja ,alituachia bara bara za uongozi pamoja na njia za kutatuwa mambo mengi ninaposema hivi ni kwamba pale alipokesea sisi ndio tunapashwa kurekebisa lakini leo naona .
    Tanzania inaanza kuaribika tunakuwa na watu wasio na heshima watu ambao hawana heshima wala uzalendo na kunavyama vya siasa vinataka kuipeleka hii nchi kwenye umwagaji wa damu ninasema hiki nikiwa nalaumu vyama vyote vya siasa vyote na ccm ndani kwanini mzee Warioba akuwa na walinzi wake mtu kama Warioba ni lazima awe na ma body guard wanne walikuwa wapi?kwa nini katika mdaharo kama huu ulinzi wa kutosha aukuwekwa? Nakwanini hawa vijana waliingia na hayo makaratasi ndani ya huu mkutano?
    Hii ni aibu aibu aibu aibu na hawa wote ni lazima wachukuliwe atuwa kali za kisheria atuwezi kuendelea na ali kama hii ,hii sio demukrasia katiba inayopendekezwa na bunge la katiba kama mnaona haifai msubiri kura ya maoni lakini sio kuipakaa nchi yetu dosari au kuipa jina baya.
    Ndugu zangu wakati umefika Raisi na serikali kuanza kuonyesha uongozi imara kabisa na hawa wenye vyama vya siasa kama na uchu wa madaraka na wenye kufikiria kutumia damu za watu kuingia ikulu it is time you need to stop you have cross the line ,
    Hawa vijana wamakamatwa video wakamatwe na waulize ninani aliwatuma ni lazima ijulikane maana katika mkutano kama huu amabao ungeweza kufungua macho ya pande mbili zote zinazopinga katiba ya Warioba na wanaoipenda katiba ya Warioba pia na katiba iliyopendekezwa na bunge la katiba, kuna mambo ambayo mzee huyo aliyasema nikaona ni kweli .
    Nina uchungu sana sana,
    Mzee warioba ni waziri mkuu mstaafu yeye na tume walifanya kazi nzuri tuu pamoja na kuwa kilamtu yuko na maoni tofauti katika katiba iliyokuwa inapendekezwa lakini ina mambo mazuri mengi asilimia 90 hawa wahuni waliokuja kuvuruga huu mkutano ni lazima wajulikane ni wakina nani ?
    Kitendo cha kutaka kumpiga ni cha ushenzi na uhuni wa ali ya juu sana wakati umefika serikali kuwajibika bila kuangalia bila chama,
    yusef

    ReplyDelete
  5. Babu Warioba alikuwa mtu wa pili baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuweza kuleta mabadiliko yoyote. Lakini pia Rais JK amempa heshima kubwa ya kuongoza tume ya mabadiliko ya katiba, kabla ya hapo hakuwahi kuongea lolote kuhusu suala hili. Tatizo ni pale anapotaka kuiteka mada ya katiba mpya kama ya kwake... Amemaliza muda wake, amelamba allowance lukuki, aache hatua zingine ziendelee. Asitake kuchukua umaarufu kwa kupitia mgongo wa JK.

    ReplyDelete
  6. Tukumbuke ya kuwa purukushani hizi zinatokea kwa kuwa Suala la Katiba linajadiliwa wakti mgumu sana ambapo tupo ktk lala salama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015!

    ReplyDelete
  7. Tuwe na utamaduni wa kusikilizana na tuache hoja ijibu hoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...