Na Anitha Jonas, MAELEZO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Profesa Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha viongozi kumi na moja aliyowateua, ambao ni Makatibu Wakuu wa Wizara ,Wakuu wa Mikoa,Mabalozi na Makatibu Tawala za Mikoa mbalimbali. Viongozi hao, waliapishwa leo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. 
 Miongoni wa viongozi walioapishwa ni aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando, ambapo amesema katika swala la upungufu wa dawa mahospitalini atajitahidi katika bajeti ijayo kujenga hoja na kutetea manunuzi ya dawa. 
 “Serikali ina mpango mbadala wa utoaji wa vifaa vya afya kwani imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kuangalia kuwepo na usawa wa gharama za huduma afya nchini,” alisema. Naye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba ameapishwa kuwa Katibu wa wizara amesema Wizara ya Maji imefanikiwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) kwa kufikia 53% kutoka 40% katika kusambaza maji safi maeneo ya vijijini. 
 Aliongeza kwamba Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mitambo ya maji Ruvu chini na kujenga visima ili kuwawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata maji ya kutosha. Aidha aliyekuwa Mtumishi Mwandamizi Ofisi ya Rais, Jack Mgendi Zoka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambapo ameahidi kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania huko na kuisaidia nchi kupata fursa nyingi na kutafuta wahisani wa kuchangia maendeleo katika taifa. Viongozi wengine, waliapishwa ni Jonny Vianney Mongela ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Hapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, ambapo amesema anaamini ushirikiano mzuri atakaoupata kutoka kwa wananchi ndiyo utakao changia mafanikio makubwa katika mkoa huo,pia kwa kupita uzoefu wake na ataenda kusimamia yote yaliyokwisha kuanzishwa ili kuleta mafanikio zaidi. Naye Bi.Amina Juma Masenza ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa , amesema ataenda kuweka msisitizo wa vipao mbele vyote vya taifa katika mkoa wake na pia amesema anaamini kufanya kazi kwa ushirikiano ndio njia ya kuleta mafanikio makubwa katika mkoa huo. 
 Wengine waliaopishwa ni Mkuu wa Mkoa Mtwara Bi.Halima Omari Dendego, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga amesema changamoto kubwa katika mkoa wake ni kupandisha pato la mkazi wa Mtwara na kupitia miradi mbalimbali iliyopo mkoa huo ikiwemo gesi kupatikana kwa mafanikio, katika swala hilo pamoja kusimamia maswala ya elimu katika mkoa huo. 
Aidha naye Samuel Shelukindo aliapishwa kuwa Balozi na kupewa wadhifa wa kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Kidiplomasia,alisema anamshukuru Rais kwa uteuzi huo na ameahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa huku akingalia maslahi ya taifa kwa ujumla. Katika hafla hiyo Makatibu Tawala walioapishwa ni Addo Mapunda na Charles Amos Pallangyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe Shelukindo anajaza  nafasi iliyoachwa wazi  na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  Mhe Liberata Mulamula, na kabla ya hapo alikuwa Afisa mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Mongela alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Denengo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Denengo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya Hapo Mhe Msengi alikuwa mkuu wa wilaya ya Moshi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha  Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...