Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha
kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya
njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore,
Maryland, Marekani.
![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland. |
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi
Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia
kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo
jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa Jumatatu,
Novemba 24, 2014 amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani Mheshimiwa
Barak Obama.
Katika salamu
zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea
vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la
tezi dume alilokuwa nalo.
Rais Obama
amesema katika salamu hizo kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini
Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika mwaka huu.
“Nakutakia
kasi ya kupona kabisa na nataraji kuendelea kufanya kazi nawe katika masuala
tuliyokubaliana ya kipaumbele”, amesema Rais
Obama kwenye salamu zake hizo.
Rais Kikwete amekabidhiwa
salamu hizo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula,
aliyekuwa ameongozana na maafisa waandamizi wa ubalozi waliofika Baltimore
kumjulia hali.
Mhe. Mulamula
amesema salamu kutoka sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zikimiminika ubalozini
kwa njia mbalimbali.
Taratibu za
matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zilikamilika Jumatatu, Novemba 24, 2014
asubuhi baada ya madaktari bingwa katika
Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland,
Marekani, kumfanyia hatua ya mwisho ya
tiba.
Rais Kikwete
ameendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na
Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea
nyumbani.
Kama kila kitu
kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea
nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais Kikwete
aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa
afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia
upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Rais Kikwete
anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona
haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
25 Novemba,2014
Mheshimiwa anaonekana ni mwenye nguvu,mchangamfu, na mwenye afya njema. Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu.
ReplyDeleteWishes you all the best, take care of your self
ReplyDeleteTunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzidi kumjaalia afya njema, Mhe. Rais wetu mpendwa.
ReplyDeleteUholanzi
Mheshimiwa pole sana,mungu akupe nguvu,wananchi wako tunakusubiri urudi,angalau utusaidie kurekebisha maana hali ya hewa imechafuka sana sakata la ESCROW.
ReplyDeleteKila la kheri mh. Rais
ReplyDeleteSeoul
Korea kusini
Mh jk pole kwa kuumwa, lakini hawa jamaa uliowachagua wakusaidie kazi wanakuangusha, njoo uwatimuwe kazi, wewe kila siku unatuangaikia wananchi wako ili tupate maendeleo
ReplyDelete