Serikali imekua ikipoteza mapato mengi kutokana na utoroshwaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee.

Kamishna wa Madini nchini,Eng Paul Massanja amesema leo wakati wa maonesho ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa ambayo yanahudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.

Amesema kwa takwimu za mwaka 2013,Tanzania ilipata dola za marekani 38 milioni wakati nchi ya Kenya ilijipatia kiasi cha dola 100 milioni na India ilijikusanyia kitita cha dola 300 milioni.

"Wote mnafahamu haya madini yanapatikana Tanzania pekee huu ni ushahidi kuwa kumekuwa na utoroshwaji wa madini haya kwa kiwango kikubwa jambo linalotunyima mapato ya kutosha"anasema Eng Massanja

Hata hivyo amesema wataendelea kudhibiti mianya ya utoroshaji wa madini nje ya nchi ambayo hayajaripiwa kodi sitahili huku kukiwa na mipango ya kujenga jengo kubwa ambalo litatumika kufanyia biashara ya madini.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Ngosi Mwihava(katikati)akikata utepe kufungua Maonesho ya Tatu ya Madini ya Vito ya kimataifa mkoani Arusha leo.
Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paul Massanja(kushoto)akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Vito jijini Arusha.
Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara kutoka nchini DRC.
Meneja Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini,Badra Masoud(kushoto) akizungumza na mmoja wa wadau wa sekta ya madini nchini,Pandit katikati ni Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Paulo Massanja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hi haikubaliki nilazima mamlaka zinazohusika zijipange! La sivyo tutabaki kujivunia Tu jina la tanzanite. Ni muhimu kujiuliza ok teknolojia ya kuchimba na kuvuna hayo madini Ni kweli hatuna lakini he Ni kweli hats uwezo WA kukusanya kodi nao hatuna! Hili halikubaliki we need to do something. New thinking New possibilities, please let us think on this!

    ReplyDelete
  2. Tunakumbuka shuka wakati kumeshakucha tayari!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...