WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itaendelea kuyalinda makabila madogo nchini yakiwemo ya Wahdazabe na Wasandawe ambayo yanategemea rasilmali misitu kwa maisha yao na ustawi wao.

“Tutakuwa tunafanya makosa kama tutawanyang’anya rasilmali misitu makabila madogo hapa nchini kama vile Wahadzabe, Wandorobo na Wasandawe kwani ndiyo rasilami pekee inayowawezesha wapate chakula cha kutosha,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Novemba 11, 2014) wakati akifungua Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Barani Afrika la Mwaka 2014 lililoanza leo kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Kongamano hilo linashirikisha wajumbe 590 kutoka ndani na nje ya nchi. Nchi za nje zinazoshiriki kongamano hilo ni 24, ambapo kati ya nchi hizo nchi 12 ni za bara la Afrika.

Kongamano hilo la siku tatu limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuwakutanisha wafugaji nyuki, wafanyabiashara, wataalamu na wawakilishi wa taasisi za ndani na nje ya nchi ili kujadili njia za kuboresha ufugaji nyuki na kukabiliana na changamoto za ufugaji nyuki hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla.

Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa Halmashauri na watu wenye maamuzi wasiwasumbue kwa kuwalazimisha wabadili maisha yao na kutoka kwenye mfumo wa ikolojia (ecosystem) ambao wameuzoea. “Tusiwabugudhi, tusiwatoe kwenye mfumo wao wa ikolojia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kabila ndogo huwa zinatoa maraisi wa Tanzania. Tofauti na nchi nyingine jirani ambapo Raisi hutoka kwenye kabila kubwa. Kwa hiyo ni wajibu wa Serikali kulinda makabila yote madogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...