Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, Said Makora (kulia), akielezea jinsi Wizara hiyo inavyopambana kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi wakati wa kongamano lililoandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Novemba 11,2014 jijini Dar es Salaam mkutano huo uliowakutanisha wamiliki wa Redio za kijamii kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ni namna gani wanavyoweza kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi ya jamii ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola, Ebola ni nini namna ya kujinga na dalili zake.(kushoto), Kushoto ni Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio FADECO, Sekiku Joseph.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
SERIKALI , Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na vyombo vya habari nchini hapa vimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwa ajili ya kuelimisha watanzania kuhusu ugonjwa hatari wa Ebola. Katika juhudi za kuwekana sawa kuhusu uelimishaji wa umma kuhusu ugonjwa huo, kumefanyika kongamano la mafunzo kwa siku mbili, Chuo Kikuu huria jijini Dar es salaam.Kongamano hilo lilifanyika Novemba 10 na 11.
Kongamano hilo liliwashirikisha viongozi wa radio za wananchi zaidi ya 28 kutoka Visiwani na Tanzania Bara. Katika kongmano hilo kulitengenezwa mikakati mbalimbali yenye kuleta uelewa kwa umma na kuwafanya kuchukua hatua za tahadhari na kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini.
Mshauri wa Redio Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ebola wakati wa kongamano hilo lililowakutanisha wamiliki wa radio za kijamii lengo ni kuwaelimsha Radio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu wanaounda kikundi kazi chenye lengo la kukabiliana na ugonjwa huo mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) . Aidha mafunzo hayo yaliwezeshwa kwa pamoja kati ya wizara ya afya na Umoja wa Afya duniani (WHO), na Shirika la kusaidia watoto la UNICEF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...