Bendi Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake lukuki kutoka sehemu mbali mbali.
Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo za kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela.
Mmoja wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA PICHA ZAIDI
ANKAL najua wewe ni mdau mkubwa wa msondo nadhani una nafasi kubwa ya kuwasaidia hawa jamaa kutengeneza DOCUMENTARY ya kipindi chote hicho na kuiuza hapa shaka itawaingizia kipato kikubwa tu. Nina amini wewe ukishirikiana na Masoud Masoud, Zomboko na Waziri Ally munawezaweza kufanikisha hili likabaki kuwa ni jambo la kihistoria. Ahsante na niwapongeze sana wana msondo kwa kutimiza miaka 50 ingawaje sikuelewa sababu ya kutoshirikishwa SIKINDE kwenye sherehe hizi.
ReplyDelete