MTANDAO
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)unaungana na watanzania kuomboleza kifo
cha mwanamuziki maarufu Hamisi Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki Jumapili
na kuzikwa Jumatatu iliyopita katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa marehemu
Amigolas atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya akiwa mwanachama wa mtandao
huo alishiriki kutafuta eneo la makazi ya wasanii ya kijiji cha Mwanzega
na shamba la wasanii lililopo Ngarambe wilaya ya Mkuranga mkoa wa
Pwani.
Alisema
alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele pale alipowahamamisha wanamuziki
wenzake kujiunga SHIWATA kutoka bendi ya African Stars 'Twanga
Pepeta'akiwemo Luiza Mbutu,marehemu Abuu Semhando na wengine.
Marehemu
Amigolas alifariki kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (M.N.H) alipokuwa amelazwa kwa siku tano kabla mauti kumkuta
Jumamosi saa tano usiku.
Mkurugenzi
wa African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka aliyekuwa mwajiri wake
kabla ya kuhamia bendi ya JKT Ruvu alisema marehemu alikuwa mwanamuzi
aliyejituma na kufanya kazi kwa juhudi zote kutoka ajiunge na bendi hiyo
mwaka 1997.
Hivi karibuni SHIWATA imepoteza wanachama wake maarufu waliofariki akiwemo Abuu Semhando,Amina Ngaluma na Muhidin Gurumo.
Marehemu
Amigolas alizikwa na umati mkubwa wa waombolezaji kwenye makaburi ya
Kisutu Jumatatu saa 10 jioni. Ameacha wajane wawili na watoto wanne.
Mungu ilaze roho marehemu mahali pema peponi. Amen.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...