Utangulizi
Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering
and Marketing (VIP)
Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.
Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.
2.0 Mauzo ya hisa za VIP
Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.
3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali
Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).
TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.
Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.
4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali
4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu
Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.
Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.
Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.
4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP
Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.
Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.
4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia
Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.
Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.
4.4 Malipo kwa mfanyakazi wa benki ya Mkombozi
Gazeti la Mawio la tarehe 20-26, Novemba, 2014 tolea namba 0122 liliandika kuwa mwanasheria wa benki ya Mkombozi ajulikanaye kwa jina la Rweyengeza Alfred alipokea malipo toka akaunti ya VIP ya shilingi milioni 40.2.
Benki inatoa tamko kuwa haina mfanyakazi anayetambuliwa kwa jina hilo na wala hakuna mfanyakazi yeyote wa benki aliyelipwa fedha toka kwenye akaunti ya VIP.
Wito kwa umma
Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.
Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.
Hitimisho
Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI
Funny if it weren't so serious! Mbona hatuelezwi uhusiano wa Benki na Bishop aliyelipwa fedha na VIP Engineering? Ama vilikuwa vijisenti na Benki imesahau? A truly Mafioso state of affairs! Mkombozi should not be worried. They won't be the fist Vatican entity to launder money!!'
ReplyDeleteSawa ila kinachofanywa ni defensive mechanism tu kama ilivyopata kufanywa na Prof. Muhongo, Prof. Tibaijuka, Maaskofu wetu na wahusika wengine wa sakata hili. Sisi wananchi tunaelewa kuwa the whole saga is is a high level technical embezzlement of the state money!!
ReplyDeleteJaribuni kusafisha kadri muwezavo lkn wananchi tunajua ukweli uko wapi
ReplyDeleteMkurugenzi mtendaji kuna swali hujajibu...kwa hiyo huwezi sema hela hazijachukuliwa kwenye magunia/ mabox.
ReplyDeleteHao ambao walipata transfer ya hela kutoka VIP account, how did they draw money from their accounts? did they do wire transfers as well!!! Kwa maana kuna argument that why should the money stay in one's account for only few hours before being drawn?
Money money money Alooooo hamjui ndiyo vijisenti vilimnunua Yesu aaaah haya ndiyo mabalaa na matokeo ya kupenda pesa....ukweli tumeujuwa..tamaa za waliowachache
ReplyDeleteTransfer ya 1(inazidi 10m) kutoka stanbic(pap a/c) kwenda Mkombozi(vip a/c) via tiss tumepewa details it was related to sales of 30% vip shares in iptl/pap.
ReplyDeleteTransfer ya 2 kutoka vip kwenda kwa watu 8 (kila transfer inazidi 10m) hatujambiwa hizo ac nane zipo bank gani naje transfer ilikua ni kwa TISS? Kama ndio kwanini sababu ya kutransfer haijabainishwa? Tunafahamu kwamba malipo yakifanyika kwa TISS au TT lazima kuena maelezo ya kwanini malipo yanafanyika. Hii imedhihirika kwenye transfer ya kwanza tumeambiwa sababu ni mauzo ya share. Maelezo yaliyo tolewa na mkombozi yako kisiasa zaidi hayakidhi kujisafisha na ashfa hii. Ni dhari transfer kwenda kwa watu 8 ilikiuka sheria za bank kuu na bank haikujiridhisha wala kutilia shaka malipo hayo.
This is a story about power, corruption and hypocricy at high levels.Yet there is an untold part! Guess what? Sex! I understand there is a paper working to disclose this as well. The juicy stuff is yet to come!!! Lord have mercy!! Stay tuned!
ReplyDeleteHon Tibajuika alijitetea, kama ana foundation, those funds would go in that account why in a personal account. So much money and nothing was said about it. I thought if someone is giving it to a charity there would be a function etc etc but we had to wait for the CAG or Tukuru to find out. Guys is there a register where politicians register gifts and what they do with it. Most countries have such a register.
ReplyDeleteGuys to show that we have no government working for us "the normal wananchi" even to feel sorry for the voters of this country, just think "is there any imaginable reason of why Mkombozi Bank and Stanbic Bank are still operating in the territory of the United Republic of Tanzania!! Enzi za Mwalimu the management of the two Banks na wahusika wote wanhekiwa KIZUIZINI.
ReplyDeleteKwani hawa siyo WAHUJUMU UCHUMI?
All in all tunataka hela irudishwa ifanye kazi ya kusaidia wananchi, viongozi, kw nn mnatumia madaraka kwa interest zenu,, na mkombozi benk sijakubaliana na maelezo yenu.
ReplyDeletechenji za ugoro, kama ugoro wenyewe ukitumia unapiga chafya inayoelekeza chafya yenye ugoro kila mahali ndiyo maana imegusa wengi waliotegemea na wasiotegemea.
ReplyDelete