MKURUGENZI WA SERIKALI ZA MITAA BWANA KHALIST LUANDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) JUU YA KUKAMILIKA KWA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MJINI DODOMA LEO AMBAPO ALITANGAZA RASMI TAREHE YA KUANDIKISHA KUPIGA KURA . (PICHA NA HABARI KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI).
====== ======== =====
Mkurugenzi wa
Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika
daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za
Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014.
Mkurugenzi huyo alisema
kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za
vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe
16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014. Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza
kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki
katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa
wanaowataka.
Alisema sifa za
mtu anayestahili kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe raia wa
Tanzania, mwenye umri wa miaka 18 au zaidi, mkazi wa eneo hilo na mwenye akili
timamu.
Pia alisisitiza
kuwa uandikishaji huo utafanyika katika vituo maalum vilivyoandaliwa ambavyo vipo
katika majengo ya umma, isipokuwa sehemu ambazo hazina majengo hayo, uandikishaji
utafanyika katika vituo maalum kutokana na makubaliano ya Msaidizi wa Uchaguzi
na viongozi wa vyama vya siasa.Bwana Luanda amesisitiza
kuwa vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 10:30 jioni.
Aidha alisema kuwa vyama vya Siasa vitaruhusiwa
kuweka mawakala wao wakati wa uandikishaji wa wa wapiga kura lakini
gharama za kuwalipa zitakuwa juu ya
chama husika. Kuhusu sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi
mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mtaa Mkurugenzi huyo alisema
kuwa ni lazima awe mtanzania mwenye umri
wa miaka 21 au zaidi na awe mkazi wa kudumu wa eneo husika.
Vile vile
alisema kuwa wasimamizi wasaidizi wa
kila kituo wanapaswa kubandika orodha ya
wapiga kura tarehe 30/11/2014, endapo mkazi yeyote au chama cha siasa kitakuwa
na pingamizi au maoni juu ya orodha hiyo basi awasiliane na msimamizi msaidizi
wa uchaguzi ili kuweza kufanyia marekebisho na orodha ya mwisho itabandikwa
siku tatu kabla ya uchaguzi.
Uchaguzi wa
serikali za Mitaa Tanzania Bara umepangwa kufanyika disemba 14, 2014, ambapo
wananchi watawachagua wenyeviti wa vijiji, vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa
Halmashauri za vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.
Viongozi
watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni pamoja na wajumbe wa
Halmashauri ya Kijiji wasiopungua 15 na wasiozidi 25, wenyeviti wa Mitaa na
wajumbe wa kamati za Mitaa wasioziidi 6 na wenyeviti wa vitongoji wa kila
kitongoji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...