Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisamiana na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu Mkurugenzi Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...