Marehemu Eng. John Said Kimbe

Jumuiya ya Watanzania Mozambique (JUWAMO) inasikitika kutangaza kifo cha Ndugu yao Mpendwa Eng. John Said Kimbe, kilichotokea ghafla usiku wa tarehe 10 Novemba, 2014 nyumbani kwake Maputo, Mozambique.

 Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa JUWAMO, Tawi la CCM Maputo, Mozambique na Mfanyakazi; Mtaalamu wa Miundombinu ya Mawasiliano “Telecommunication/ICTs expert” kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), kitengo cha “Southern Africa Telecommunications Association (SATA) tangu Juni 2001.  

Jumuiya ya Watanzania Mozambique inawafahamisha Watanzania wote waishio Jiji la Maputo na vitongoji vyake kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa “Memorial Service” tarehe 13 Novemba, 2014 katika Kanisa la Roman Catholic “Paroquia Nossa Senhora das Victoria” Karibu na Soko la Janet – Maputo, saa 9. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanzania kwa mazishi tarehe 14 Novemba, 2014.

JUWAMO inawaomba Watanzania wote kujitokeza kumuaga mpendwa wetu na kuwafariji wafiwa kama mila na desturi zetu zinavyotuelekeza.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Katibu wa JUWAMO Ndugu Annuar Aziz Simu No. +258824034391 au +258842337117 na Katibu wa CCM –Tawi la Maputo, Mozambique Ndugu Gesona Ngabo Simu No. +258821403433.
Imetolewa na JUWAMO

12/11/2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu ailaze pema roha ya marehemu Kimbe Amen...

    ReplyDelete
  2. Innalillah wa innalilahi rajiuuna. Kila nafsi itaonja mauti.

    ReplyDelete
  3. RIP Dady
    Isaelly

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...