Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umekuwa Mshindi wa kwanza miongoni mwa taasisi
za serikali na mashirika ya umma yanayofanya manunuzi makubwa nchini na hivyo
kutunukiwa tuzo ya uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi kwa kipindi
cha mwaka 2013/2014.
TASAF
imekuwa miongoni mwa taasisi zilizoshinda tuzo ya ubora wa manunuzi kwa nchi za
Afrika Mashariki kwa mwaka 2013/2014 na kukabidhiwa tuzo katika hafla
iliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya ambako Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.
Ladislaus Mwamanga aliipokea tuzo kwa niaba ya taasisi hiyo ambayo kwa sasa iko
katika jitihada kubwa za kulisaidia taifa kuondokana na umaskini kupitia mpango
wake wa kunusuru kaya maskini PSSN.
Akizungumza
baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus
Mwamanga amesema licha ya taasisi yake kufanya
manunuzi makubwa kutokana na uwingi wa shughuli za kutekeleza Mpango wa
Kunusuru Kaya maskini, kanuni, taratibu na sheria za manunuzi ya umma zimekuwa
zikizingatiwa kwa kiwango kikubwa. Bw. Mwamanga amesema kwa takribani miaka
mitatu mfululizo TASAF imekuwa ikipata hati safi ya manunuzi na kuwa miongoni
mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma zinazofanya vizuri katika uzingatiaji
wa sheria ya manunuzi nchini.
Zifuatazo ni picha za
upokeaji wa tuzo hiyo zilizofanyika Nairobi-Kenya
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (mwenye
Kaunda suti) akiwa na ngao ya ushindi wa
kwanza ya uzingitiaji wa kanuni za manunuzi nchini kwa mwaka 2013/14
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga
(kushoto) aliyeshika ngao ya ushindi wa
kwanza (kulia kwake) ni Mwenyekiti wa
Bodi ya PPRA Bw. Marten Lumbanga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Susan
Mlawi (kushoto) alikuwa miongoni mwa
wageni walioalikwa kwenye hafla ya kukabidhi
tuzo ya manunuzi kwa taasisi za Serikali na mashirika ya umma kwa nchi
za Afrika Mashariki iliyofanyika mjini Nairobi, Kenya
Baadhi ya viongozi wa taasisi zilizo
shinda tuzo ya manunuzi kwa mwaka 2013/14 kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...