Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava akizungumza kabla ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa pili kulia), Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa pili kushoto), na maafisa wengine kutoka TMAA, Eng. Charles Shamika (wa nne kushoto) na Flora Kisena (wa kwanza kushoto).
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa nne kulia), akisoma moja ya zabuni (bid) ya ununuzi wa madini yaliyokuwa yakipigwa mnada jijini Arusha. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava (wa tano kulia), Zabibu Napacho, Afisa Mfawidhi Ofisi ya TMAA-Arusha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari TMAA, Eng.Yisambi Shiwa (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa tatu kulia), Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa pili kushoto), na Eng. Charles Shamika (wa nne kushoto), Flora Kisena (wa kwanza kushoto) kutoka TMAA.
wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, wakishuhudia mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi bila kuwa na vibali husika.Aliyenyanyua karatasi ya maombi ya zabuni (bid) ya madini hayo ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta.
Meneja Usafirishaji Madini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), George Kaseza (katikati),akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, mara baada ya kumalizika kwa mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Na Teresia Mhagama

Madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliyokamatwa wakati yakisafirishwa nje ya nchi bila kufuata taratibu za nchi za usafirishaji madini yamepigwa mnada na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

Madini hayo yamepigwa mnada jijini Arusha katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru ambapo mnada huo wa kwanza kufanyika nchini ulishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava, Mwenyekii wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesera, Makamishna Wasaidizi wa Madini nchini na wananchi waliohudhuria maonesho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...