Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dk. Mwajuma Mbaga (kushoto) akipokea msaada wa mabechi ya kukalia wagonjwa wakati wakisubiri huduma kutoka kwa Kaimu Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL),Bw. Edwin Mashasi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano,iliyofanyika leo Novemba 19,2014.
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dkt. Mwajuma Mbaga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa kituo hicho.Kulia waliokaa ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TTCL Bw. Edwin Mashasi.
Sehemu ya mabenchi yaliyotolewa na kampuni ya simu Tanzania (TTCL). Msaada huo umegharimu shilingi milioni moja na laki saba.
Wafanyakazi wa kituo cha afya Buguruni katika picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...