Picha ya pamoja, Baadhi ya wana kikundi cha UWF, mwakilishi kutoka Tanzania Women Bank (TWB), Bi Khadija na Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakiwa katika picha pamoja.
 Pichani kulia ni Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) Mikocheni jijini Dar,mwishoni mwa wiki,kuhusiana na hafla fupi ya kumkumbuka Marehemu Aziza Mbogolume,ambaye alikuwa mshindi wa kwanza wa shindano la MWANAMAKUKA 2013.
Shindano hilo huandaliwa na kikundi cha UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF),kupitia mradi wao wa MWANAMAKUKA, hafla hiyo pia iliwakutanisha wadau mbalimbali wa kikundi hicho wakiwemo na washindi wa mradi huo ambao umekuwa ukifanya vyema kila mwaka,Anaefutia pichani ni Bi Jane Magembe, , Mwate Madinda na Martha Kalaghe. 
Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo,akionesha moja ya, kipaji cha marehemu Aziza, ambacho kilikuwa ni uchoraji.
 Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakijadiliana jambo,ambapo walikukutana kwa madhumuni ya kumkumbuka Mwanamakuka mwenzao aliyefariki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...