Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi aongoza zoezi la kupima afya za Wabunge katika Ukumbi wa Msekwa jana.Upimaji wa afya za Wabunge umefanywa na Madaktari wa Aga Khan kutoka Morogoro,Dar. na Dodoma.
Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Agha Khan,Sisawo Konteh wakati wa zoezi la upimaji wa Afya kwa Waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.Katikani ni Mmoja wa Maafisa waandamizi wa Hospitali ya Agha Khan.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Mchungaji Luckson Mwanjale akimsikiliza kwa Makini Mtaalam wa Maswala ya Afya kutoka Hospitali ya Agha Khan wakati wa zoezi la kupima Afya kwa waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akijiandaa kupima uzito wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma akipima akichukuliwa vipimo na Daktari kutoka Hospitali ya Agha Khan.
They should not be gettin freebbie, these people are very highly paid!!
ReplyDeleteWiki iliyopita malipo mapya ya kulazwa na chakula Muhimbili yalisimamishwa kwa sababu yalikuwa ya juu kwa wagonjwa wa kawaida. Kuendesha hospitali yoyote ni gharama kubwa wizara iangalie uwezekano wa malipo hayo kubaki kwenye daraja la Kwanza/private la Muhimbili kwa wale wanaoweza kujilipia. Ukweli ni kwamba wapo watanzania wanaoweza kuchangia wengine wanajipeleka India na sehemu nyingine za dunia.
ReplyDelete