·         Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10.
·         Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali” imeandaa
 matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia 
elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati 
shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.
Matembezi
 hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau 
mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa
 moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.
Akiongea
 kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema 
“wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na 
kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa 
njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari 
ameshachangia.
Na
 sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, 
marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha
 watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri
“Lengo
 ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na
 kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”  
Tutafanya
 Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze 
kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana 
katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa 
kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.
Tunatoa
 wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi 
haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi 
ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora 
,katika mazingira mazuri  na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa
Airtel
 chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi 
katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa 
wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king 
Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi 
imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili 
ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu 
ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...