Bw. Noel
Kaganda, Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, New York; na Bw. Suleiman Saleh, Afisa katika Ubalozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C wakiwa na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha La Verne cha California waliotembelea Ubalozi wa
Tanzania Washington D.C. kujifunza namna Tanzania inavyoshiriki katika Umoja wa
Mataifa. Wanafunzi hao walipeperusha bendera ya Tanzania katika National Model
United Nations (NMUN), iliyofanyika kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 2 Novemba
2014, huko Washington D.C.
Bw. Kaganda, akiwasilisha mada kuhusu ushiriki
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na
vipaumbele vya nchi katika vyombo, kamati, kamisheni, bodi na mikutano ya nchi
wanachama wa mikataba mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Programu ya NMUN inatoa
fursa kwa wanafunzi wa vyuo zaidi ya 5000 kutoka pembe zote za dunia kuvaa
kofia za Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa na kujadili changamoto mbalimbali
zinazoikabili dunia, ikiwemo migogoro, mabadiliko ya tabianchi, maafa, janga la
umaskini, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na usawa na uwiano sawa wa
kijinsia. Mafunzo haya kwa vitendo yanawajengea uelewa wa shughuli za Umoja wa
Mataifa na kuwapatia kionjo cha shughuli
za kidiplomasia.
Washiriki
wakifuatilia kwa makini mada inayowasilishwa. Pamoja na taarifa za kiuwakilishi
katika Umoja wa Mataifa, wanafunzi hao walipata wasaa wa kufahamu misingi na
mikakati ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania iliyojikita katika kuendeleza
mahusiano ya kiuchumi na kibiashara na kukuza fursa za uwekezaji.
Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Uwakilishi wa Kudumu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa zinaendelea kupokea
wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali vya Marekani ambavyo vimeonesha kiu
ya kupata uelewa wa shughuli za kidiplomasia na habari za vivutio vya kiutalii vilivyopo
nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...