MPANGO Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) unatoa rai kwa wananchi
wote wenye sifa za kuchangia damu wajitokeze kuchangia damu katika vituo
vya Damu salama hasa kipindi cha mwezi Novemba mpaka Januari mwakani ,
kipindi ambacho wanafunzi wa sekondari wanakuwa likizo hivyo kusababisha
kuongezeka kwa uhaba wa damu nchini.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Habari wa Mpango wa Taifa wa
Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda (pichani) katika mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika ilala mchikichini, Dar es salaam, alisema damu salama kwa
kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama
cha Msalaba Mwekundu umekusanya chupa za damu asilimia 97% na kuvuka
lengokatika kipindi cha miezi mitatu julai hadi septemba 2014.
Jumla ya chupa 40,974 zilikusanywa , lengo lilikuwa kukusanya chupa 42,500.
\“Katika kipindi hicho chupa za damu zilizokusanywa toka vituo vidogo( Blood
collection satellite sites) ni 2,886 (8%) ambapo kituo cha Morogoro chupa 1,158,
Dodoma-818, M/moja-490, kigoma- 93 na Lindi-327)” alisema.
Alisema katika robo mwaka ya Julai- Septemba 2014 asilimia 32 ya jumla ya
chupa zilizokusanywa zilitengenezwa mazao ya damu; Packed Red blood cell,
chembe sahani (platelets) na plasma. Lengo lilikuwa ni kutengeneza 40% ya damu
iliyokusanywa.


.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...