Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt
Injinia Binilith Satano Mahenge akifungua rasmi Kongamano la ukuaji wa uchumi
unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi kwa
niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed
Gharib Bilal,itakayofanyika kwa muda wa
siku mbili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt
Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) ,kuhusu umuhimu wa Kongamano hilo lililoandaliwa na
Benki Kuu ya Dunia kwa ushirikianao na Ofisi ya Makamu wa Rais. Anayefuatia wa
pili kulia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na
Mazingira Mhe. James Lembeli, Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Philippe Dongier (kulia) pamoja na Bw.Vel
Gnanendran Mkuu wa Ofisi ya DFID nchini Tanzania.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ndg. Sazi Salula
(katikati), akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), pamoja na
Mkurugenzi Msaidizi - Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt.Richard Muyungi
katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Washiriki kutoka Nje na ndani ya Nchi wakisikiliza
kwa makini hotuba inayotolewa na mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -
Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi waliohudhuria katika Kongamano
la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi .
======= ======= =======
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia
Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta
nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu. Aliyasema
hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya
Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam. Alifungua Kongamano hilo kwa
Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib
Bilal.
Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo
zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira. Aidha alisema kuwa
zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika
kuhakikisha utunzaji wa mazingira
unatekelezwa na pia kuzuia uharibifu wa
mazingira kwa njia moja au nyingine.
Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia
Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa
ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza
kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania
hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.
Mwisho Waziri Mahenge aliwashukuru Wadau mbalimbali ambao
wamehudhuria kongamano hilo kutoka ndani na nje ya Nchi. Akiwasihi sana
kuendelea kutunza mazingira na pia aliwaomba watembelee vyanzo mbalimbali vya
Utalii vilivyopo Nchini Tanzania ili kukuza uchumi .
Kongamano hilo ni muendelezo ya Mkutano wa New York kuhusu
mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu na limehudhuriwa
na washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...