Frank Mvungi-Maelezo
Watanzania wametakiwa kuendeleza amani na mashikamano uliopo kwa
maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa kuenzi misingi ya Amani na
Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge
Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa
shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.
Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu wachache hivyo ni lazima
tuwaepuke wote wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo
alisema Mpanju.
Akifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja ya midahalo
iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa na watu
wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo
vinaweza kuleta madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama
walemavu,wanawake na wataoto.
Akizungumzia Katiba inayopendekezwa Mpanju amesema ni vyema
Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na
baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.
Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka kauli zinazoweza kuleta uchochezi
katika jamii hasa katika kipindi hichi ambapo baadhi ya watu
wamekuwawakitumia mwavuli wa Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu
Katiba inayopendekezwa na kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa
amani.
Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kupinga
vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani hapa nchini kwa
kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya Taifa na si ya Kikundi
Fulani cha watu.
Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha kuhusika na vurugu zilizotokea
katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es salaam na kudai hahusiki na tukio
hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .
Aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju
ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye
ulemavu Tanzania akiwaeleza waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa wazalendo na kulinda
amani iliyopo hapa nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...