Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi wa   Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano  huo ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani  chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka  Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.
Mhe. Membe akikaribishwa na Prof. Florence Luoga ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii  ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo
JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Waziri Membe, naomba nikuulize, swala la uraia pacha limeishia wapi? Nchi kadhaa za kiafrika wanaruhusu dual citizenship, Kenya, Ghana, Rwanda, etc, etc, ... Kama Tanzania iko tayari kumpa uraia mgeni ambaye nchini kwake alikotoka wanampa uhuru wa dual citizenship, kwanini tunamnyima mtanzania haki ya uraia wa nchi yake.

    ReplyDelete
  2. Passipoti ya Tanzania niya kijani iliyokolea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...