Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa kwanza wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Jassim M. Al-Darwish alipokwenda kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Waziri Membe akizungumza jambo na Balozi Jassim M. Al-Darwish huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (kushoto) akisikiliza.
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akisikiliza mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Al- Darwish ambao hawapo pichani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...