Timu ya Yanga leo imefungwa 1-0 na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba katika Ligi Kuu ya Vodacom, mjini Bukoba, Kagera.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Klabu ya Dar es salaam Young Afrika imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Kipindi cha kwanza Timu zote mbili zilimaliza bila ya kufungana, Kipindi cha pili Kagera Sugar walitumia faida ya kucheza nyumbani na kufanikiwa kupata bao lililofungwa kiufundi na paul Ngwai na kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 na kuwaacha Yanga wakibaki na pointi zao 10 ambazo wamevuna katika michezo 6.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...