Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku
Zanzibar, Zanchick, leo imetoa chanjo 600,000 zilizo na thamani ya Tshs 9,000,000
kwa wafugaji kuku kwa ajili ya kuwalinda kuku wao na ugonjwa wa Mdondo.
Utoaji wa chanjo hizo ulifanyika kwa msaada wa wizara ya Ufugaji na Uvuvi
Zanzibar ambao wata ratibu na kusimamia zoezi zima.
Meneja wa Uendeshaji, kutoka Zanchick, Bwana Christopher Kontonasios alisema:
“Tunashukuru Wizara ya Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa washiriki wakubwa katika
kuratibu zoezi hili na tunataraji serikali itazidi kuwasaidia wazalishaji kuku
wa kawaida, kwa kuondoa kodi ya kuagiza chakula cha kuku, jambo ambalo
litawaruhusu wazalishaji wa kawaida kupata chakula bora cha kuku chenye bei nafuu.
Hii ndio njia pekee ya kuwawezesha wakulima wa kawaida kuendeleza ufugaji wa
kuku, kwa kiwango cha hali ya juu, na pia kuwaruhusu kukidhi biashara zenye faida.
Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya
Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis alisema, “Tunafarijika na juhudi
za Zanchick katika kuboresha uzalishaji wa kuku Zanzibar, hii ni hatua kubwa kwa
wafugaji wa kawaida. Tunatarajia kuongeza juhudi katika kushirikiana kukuza
viwango na jitihada za ufugaji kuku kisiwani hapa."
Kirusi cha ugonjwa wa Mdondo kwa ujumla hakisababishi madhara yoyote kwa afya
ya binadamu, lakini kina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwa wafugaji wa kawaida,
kwa kumaliza kiasi kikubwa cha kuku na hatimaye kuangamiza biashara yao.
Msaada huu mkubwa na muhimu ni katika juhudi za Zanchick kufanya kazi na
wafugaji wa kawaida ili kuongeza, kuboresha na kunadi uzalishaji wa kuku Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar(Zanchick) Bw.Issa Khasim Issa akikabidhi chanjo 600,000 zenye thamani ya Tshs 9,000,000 kwa Naibu katibu katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Omar Ali Amir kwa ajili ya kuwalinda kuku na ugonjwa wa Mdondo, anayeshuhudia kulia Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...