
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kama ishara ya kuzindua huduma za maji kwa wakazi wa kijiji cha Mpigamiti, mradi huo utahudumia vijiji vingine viwili vya Namakololo na Mitawa ambapo wakazi zaidi ya 6000 watafaidika na mradi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi.Hadija Sheweji mkazi wa kijiji cha Mpigamiti mara baada ya kukagua mradi wa maji.
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mangirikiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.
PICHA ZAIDI BOFYA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...