Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa bwana Kharist Michael Luanda akitangaza idadi ya watanzania waliojiandikisha kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ijayo.
Jumla ya Watanzania 11,491,661 sawa na asilimia 62% ya watanzania 18,587,742 ambao
walitarajiwa kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ijayo
wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa
mikoa ambayo imeandikisha idadi kubwa ya wapiga kura ni Katavi 79% na Kagera (78%) na
mikoa ambayo iliandikisha idadi ndogo ya wapiga kura ni Dar es salaam 43% na Kilimanjaro
50% .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...