Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa na baadhi ya Wahitimu wa Kituo cha Chekechea cha Florence cha Kigogo Dar es salaam.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala  akizungumza katika Mahafari ya Kituo cha Chekechea cha Florence yaliyofanyika Kigogo Dar es salaam. Watoto mia moja wamehitimu katika Kituo hicho na wote wamejifunza na kuelewa  kusoma na kuandika.
Balozi Kamala amewashukuru Bwana na Bibi Mbezi kwa kuanzisha kituo hicho. Aidha, Balozi Dr. Kamala ameanzisha mfuko wa zawadi wa Dr. Kamala "Dr. Kamala Award Fund" utakaokuwa unatoa zawadi kila mwaka kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Baada ya Balozi Kamala kutoa laki moja za kuanzisha mfuko huo wazazi walimuunga mkono kwa kuchangia laki moja.
Balozi Kamala amehaidi kuchangia milioni moja mfuko huo na riba itakayopatikana kila mwaka itatumika kutoa zawadi kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Vile vile Balozi Kamala alichangia shilingi laki mbili na nusu kituo hicho na amehaidi kukitafutia wafadhili wa kukisaidia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aisee yaanin mchango wenyewe laki moja tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...