Wiki iliyopita tarehe 17-18, Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii, uliandaa kongamano la uwekezaji katika sekta ya utalii, kwa nia ya kuvutia wawekezaji na watalii ili kuongeza idadi kubwa ya watalii wanao kwenda kuitembelea Tanzania.
Ubalozi Mdogo umejiwekea utaratibu katika mpango wake wa mwaka, kuandaa kongamano za uwekezaji tatu kwa kila mwaka.
Ni imani kuwa mpango huu utasaidia kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuvutia idadi kubwa ya watalii kuitembelea Tanzania na vivutio vyake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...