Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto)
akiagana na Balozi wa Australia nchini anayemaliza
muda wake, Geoff Tooth.
Balozi
Geoff Tooth (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava
ambapo Balozi huyo alimshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka katika Wizara
na kumhakikishia kuwa Serikali ya Australia imedhamiria kuuenzi ushirikiano huo
ambao ni wa kihistoria. Alisema Tanzania ijiandae na uwekezaji mkubwa kutoka
kwa kampuni kubwa za Australia hususan katika masuala ya mafuta na gesi asilia.
Naibu
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava (katikati) katika
picha ya pamoja na Balozi Geoff Tooth (wa pili kutoka kulia). Wa kwanza kushoto
ni Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje katika Idara ya Asia na Australia, Bertha
Makilagi, anayemfuatia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius
Mwenda kutoka wizara ya Nishati na Madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...