Mdhibiti Uhalifu
wa Kifedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Thomas Mgonja (kushoto)
akikabidhi msaada wa sabuni kwa Enesi Sanga ambaye mtoto wake amelazwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wafanyakazi wa idara ya udhibiti wa
uhalifu wa kifedha ya benki hiyo walikwenda hospitalini hapo jijini Dar
es Salaam jana kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni
sehemu ya mpango wa NBC wa kuhudumia na kurudisha sehemu ya faida
waipatayo katika shughuli za kijamii.
Mdhibiti Uhalifu
wa Kifedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Thomas Mgonja (kushoto)
akikabidhi msaada wa sabuni kwa Flora Mgawa ambaye mtoto wake amelazwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wafanyakazi wa idara ya udhibiti wa
uhalifu wa kifedha ya benki hiyo walikwenda hospitalini hapo jijini Dar
es Salaam kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni sehemu ya
mpango wa NBC wa kuhudumia na kurudisha sehemu ya faida waipatayo
katika shughuli za kijamii.
Ofisa
Miradi wa asasi ya Tumaini la maisha Tanzania, Meshack Nyambele (kulia)
akipokea sehemu ya misaada ya vitu mbalimbali kutoka kwa Mdhibiti Uhalifu
wa Kifedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Thomas Mgonja
vilivyotolewana benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...