Lorietha
Laurence -Maelezo.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo
ametoa wito kwa kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze
kuhakikiwa na kulipiwa kwa kupata kibali
cha kuingia sokoni kama sheria ya filamu
ya mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.
Akizungumza katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es
Salaam, Fisoo ameipongeza kampuni ya
Al-Riyamy Production ambayo imeweza kutimiza
wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa stamp
za TRA na hivyo kuwa tayari kuingia
sokoni. Aliongeza
kuwa kuna baadhi za kampuni za filamu
nchini zimekiuka utaratibu na kushindwa kuwasilisha filamu zao kwa Bodi ikiwemo
filamu zile zilizoigizwa miaka ya zamani
ambazo zimekuwa zikionyeshwa bila kibali.
“Nimefurahishwa sana kwa namna ambavyo kampuni ya Al-Riyamy Production kwa kufuata sheria na kanuni za
filamu nchini, hivyo natoa wito kwa kampuni nyingine pia kuweza kufanya hivyo ili kukuza uchumi wetu na wao waweze
kufanya biashara bila usumbufu” alisema Fisoo.
Naye
mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee
Jangala, amewaomba wasanii wenzake wenye kampuni za filamu waweze kufuata
taratibu na sheria za bodi ya filamu ili kukuza soka la filamu na kuinua uchumi
wa nchi yetu.
“Nawasiii
wasanii wenzangu na wamiliki wa kampuni za filamu nchini waweze kufuata sheria
na kanuni za filamu ili tuweze kwenda vizuri kwa kila mmoja kutimiza wajibu
wake katika ulimwengu huu wa filamu” alisema Mzee Jangala.
Baadhi
ya kampuni ambazo zimeweza kuwasilisha kazi zao katika Bodi ya filamu ,ni
pamoja na kampuni ya Wananchi wote
wamewasilisha filamu 119, Game First Quality filamu 35, steps Entertainment
filamu 739, na Al-Riyamy Production
filamu 134.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo akiamwandikia kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) akimuonyesha stakabadhi ya malipo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo baada ya kufanya malipo ya kupata kibali kwa ajili ya filamu za kampuni hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo akimkabidhi kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu,leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Simon Peter (kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu wanaotazama ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(katikati) na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo (kushoto) ,leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).
Isiishie kuwasilishwa katika Bodi tu, pia hiyo Bodi ihakikishe filamu zinahakikiwa (edit) lugha iwe ni Kiswahili ama Kiingereza. Filamu zetu lugha ni ovyo sana (hasa tafasiri za Kiingereza). Ni aibu tupu, ukizingatia siku hizi zinaonekana katika baadhi ya chaneli za kimataifa!
ReplyDelete