Jumatatu tarehe 1-12-2014 Excutive Chef Issa Kipande maarufu kama Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuonana na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe.  Dorah Msechu pamoja na Wafanyakazi wote wa ubalozi ambao walimpokea kwa furaha sana na kumpa pongezi nyingi wakijivunia ushindi alioupata nchini Luxembourg kwenye Mashindano ya Chef's World Cup 2014.
Chef Issa ameiambia Globu ya Jamii leo kuwa  alifarijika sana kwa upendo, heshima na ushirikiano alioupata toka kwa Mheshimiwa balozi na wafanyakazi wote wa ubalozini hapo.
"Inatia hamasa sana ya kuendelea kufanya mambo mazuri zaidi kutokana na mchango wa mawazo pamoja na kutambulika na kuheshimika kwa juhudi na mafanikio binafsi yanayoiletea sifa nchi yetu Tanzania. 
" ASANTE SANA MAMA MHESHIMIWA BALOZI DORA MSECHU MOLA AKUJAALIE WEWE NA WAFANYAKAZI WOTE HAPO  UBALOZINI MAISHA MAREFU YA FURAHA NA AFYA NJEMA AMEEN UENDELEE KUTUWAKILISHA WATANZANIA TUNAOISHI SWEDEN " alisema Chef Issa.

Akaongezea: "Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaliia kushiriki chef's world cup inafanyika kila baada ya miaka mnne kama football  world cup.

"Ni heshima kubwa sana kwa nchi yangu nimeitendea haki nchi yangu kwa kupata tuzo ya mafanikio na badges ya utambuzi na first world touch smartwatch ooohhh baada ya timu nilivyokua nayo kushinda kombe la dunia la mapishi pia nimeandika historia ya kuwa Mwafrika  na mweusi pekee kushiriki mashindano haya. Nawashukuru sana wote mnaoniunga mkono kwa namna moja ama nyingine. Tupo pamoja ndugu zangu. Na ninaahidi kuwa sitawaangusha kamwe..."

Ili kusoma habazi zilizopita pamoja na taarifa ya ushindi wa Chef Issa alioupata akiwa na Timu ya Stockholm iliyonyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda (Regional teams) BOFYA HAPA

Executive Chef Issa Kipande akiwa nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden.
Executive Chef Issa Kipande akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea Ubalozini hapo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dorah Msechu baada ya kumpokea shujaa huyu hapo ubalozini.
Executive Chef Issa Kipande akiwa pamoja na Balozi Dorah Msechu anayeshikilia kwa furaha na fahari medali ya ushindi  ya Chef Issa.

Kupata mambo mengine kibao hebu M-Like 
Chef Issa kwenye Facebook page yake hapa chini...
https://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534?fref=ts




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Huyu Chef Issa aanzishe mikahawa ya kimataifa Dar Arusha na Mwanza na sisi wenyeji tujifunze kula kwenye mikahawa mara kwa mara ili tuinue biashara zinazoweza kuongeza ajira katika sekta ya huduma.

    ReplyDelete

  2. Big up chef Issa , Paaaaa tu kwa raha zako unastahili

    ReplyDelete
  3. FAHARI YA TANZANIA KWA WIZARA HUSIKA, HONGERA SANA MUHESHIMIWA BALOZI DORA MSECHU KWA KUMTAMBUA KIJANA NA KUMKARIBISHA UBALOZI WEWE NI MFANO WA KUIGWA SAFI SANA

    UK

    ReplyDelete

  4. Duh Chef Issa umeshusha dua la nguvu kwa mama balozi hahahaaaaa lakini anastahili pongezi na dua hizo pia inafariji na kufurahisha sana pale juhudi binafsi inapopata heshima na kukubalika wewe sasa ni kioo cha jamii naimani wazazi waliopata nafasi ya kuona mafanikio yako watawaunga mkono watoto wao ili waweze kupambana nao wafikie au wazidi ulipo wewe chef Issa.

    Hongera sana

    Netherland

    ReplyDelete

  5. Ubalozi wa Tanzania Sweden mmefanya jambo la maana sana wote tumefurahi na mmetuwakilisha vyema watanzania woote kijana kaibeba nchi yetu juu zaidi.

    Mdau Geraman

    ReplyDelete

  6. UPISHI ULIKUA UNADHARAULIKA SANA DUH SASA TUNASHUHUDIA MTANZANIA ANAFANYA MAAJABU KWENYE KOMBE LA DUNIA HII KIBOKO HIVI NI MATANZANIA GANI AALISHINDANA KWENYE KOMBE LA DUNIA? UKIACHA KINA NYAMBUI WALIOSHINDA KWENYE OLIMPIKI MIAKA HIYO CHEF UMETISHA

    ReplyDelete

  7. Mapochopocho tu na mahanjumati yamekufanya kijana unaheshimika si mchezo kila juhudi walah inalipa komaa mdogo wangu safari ndio imeanza utafika mbali sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...