Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa la Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha mungu kwa njia ya uimbaji 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama. 

Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo. 

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...