Mechi ya Nani Mtani Jembe namba 2 inachezwa jioni hii ya leo Jumamosi Desemba 13,2014 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo inawakutanisha Watani wa Jadi timu za Yanga dhidi ya Simba SC zote za jijini Dar.
Hadi hivi sasa tunaingia mitamboni Simba inaongoza mabao 2- 0 yaliyotiwa kimiani na Wachezaji Awadhi Juma (dk 30) aliewahi mpira wa faulo uliopigwa na Mshambuliaji Emmanuel Okwi baada ya Kipa wa Yanga,Munishi Dida kuutema,Goli la pili lilifungwa na Elius Maguli (dk 41).

Kipindi cha pili cha Mchezo kimeanza na Timu ya Yanga walitawala mpira dakika zote za mwanzo wamepoteza nafasi nyingi za wazi, Na kwa upande wa Mashabiki wa Yanga hali ishakuwa tete na wengi wameanza kutolewa kwa machela wakiwa wamepoteza fahamu.

Mpira umeisha na Simba wanatoka kifua mbele kwa bao 2 - 0 

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Umechemka uncle

    ReplyDelete
  2. Mtaamini Simba wenzangu kuwa gazeti la Nipashe mtandaoni halikutaka kuripoti ushindi wetu?
    Nami nilijua hivo na sababu ni dhahiri!!
    Prior to last night niliamua kugomea kulisoma gazeti hilo kutokana na tabia yake ya kuibeza timu yetu.
    Na itafika wakati watapiga marufuku hata kutumia jina 'Simba' gazetini mwao.
    Hongera wana Msimbazi!!

    ReplyDelete
  3. MANJI MPIRA UMEKUSHINDA HUNA UNACHOISAIDIA YANGA WE UNGEANZA TU

    ReplyDelete
  4. Umechemka sana list ya wliocheza inatisha? Hadi Kavumbagu, KiizA Domayo Tambwe Luende wamecheza, kweli hii mtani jembe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...