Vijana wa Kikundi cha “Hisia Theatre Group” wakionesha ujuzi wao wa sarakasi wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini leo Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) Hamisi Tika kwenye banda la PPAA wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...