
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET) Bi. Asha Baraka amethibitisha hilo na kusema kwamba mwili ndiyo ulikua unapelekwa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.
“Mjomba wa marehemu amejaribu kuwaomba sana Polisi waache kuuchunguza mwili wa Aisha kwani wamemshukuru Mungu kwa yote lakini wamekataa hivyo hadi watakapomaliza kuchunguza ndipo watatupa mwili” alisema Asha.
Kifo cha Aisha ambacho kimejaa utata kutokana na jinsi kilivyotokea kwani hakuwa akiumwa na alikutwa amelala kibarazani kwa rafiki yake Samira Saleh huko Mabibo Jijini Dar es Salaam.
Hata mtoto wake wa kiume Said alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kwamba mwili wa mama yao ulipelekwa hospitali na mwanamke ambaye hata wao hawamfahamu na hapo ndipo panapoleta utata.
Kifo cha Aisha kimethibishwa na Kamanda wa Kanda ya Polisi Mkoa wa Kinondoni Camillius Wambura.
Juzi majira ya saa mbili asubuhi Aisha alikutwa na rafiki yake Samira Saleh akiwa amelala usingizi mzito kibarazani nyumbani kwake Mabibo (nyumbani kwa Samira).
Marehemu Aisha anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwao Mikadi Beach Kigamboni baada ya swala ya Ijumaa.
It is so sad, she is very young and full of life. Rest in peace
ReplyDelete