Timua timua ndani ya Yanga imeibua kadhia kubwa ambapo zaiodi  ya TSh  bilioni 3 ndani ya klabu hiyo zikidawia kuchotwa na kwamba uchunguzi unaendelea. 
Mwanasheria wa Yanga George Chacha ameiambaia
Globu ya Jamii kwamba  pamoja na kuwa ukaguzi bado unaendelea lakini huenda kuna mabilioni ya fedha yakawa yameyeyuka  ndani ya klabu hiyo. 
Alisema: "Kwa haraka haraka kuna fedha kiasi cha dola 2500 za tiketi ya mke wa aliyekuwa kocha msaidizi  Leonado Neiva, aliyetakiwa atumiwe ili aje, hizo hela zimetoka lakini hazikufanya kilichokusudiwa, na makocha ndio kama hivyo wametimuliwa. 
"Kuna fedha pia za Marcio Maximo kiasi cha dola 21 milioni (sawa na 35,700,000 za Tanzania) ambazo ni kodi ya nyumba na masuala mengine. Hizo hela pia Maximo hakupewa. Sasa wakati wanakatishiwa mikataba ndio ikagundulika -  fedha zimetoka lakini hazikufikia walengwa wala kufanya kilichotakiwa."alisema Chacha. 
"Yanga kama sio kufukuzwa makocha hao sidhani kama ingebainika mapema hivi kuwa kuna hela zimepigwa. Kuna watu wanapiga hela. Hela zinatolewa lakini hazifiki zinapostahili." 
Yanga iliwatimua Maximo na msaidizi wake Neiva mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni pamoja na kiungo mkabaji Mbrazil, Emerson Oliveira Neves Roque baada ya mchezo wa Nani Mtani Jembe ambapo Yanga ilinyukwa mabao 2-0.
"Kuna mambo mengi sana. Ukaguzi unaendelea. Utakapokamilika kila kitu tutaweka wazi na watakaogundulika wamehusika kwa namna moja au nyingine hatua zitachukuliwa,"alisema.
 Kuhusu kushikiliwa kwa mahojiano kwenye kituo cha Polisi Central kwa aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga Benno Njovu na mkuu wa idara ya fedha Rose Msamila, Chacha alisema "Ni kweli juzi Ijumaa saa 11 jioni ndio walichukuliwa kwa mahojiano na kuruhusiwa, kama ninavyokwambia uchunguzi bado unaendelea,"alisisitiza.
Juhudi kubwa za kuwasaka Njovu na Rose lakini hawakupatikana baada ya simu zao za kiganjani kutokuwa hewani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...