Katika
pita pita zetu za Mtaa kwa Mtaa,tuliibuka maeneo ya Tabata Matumbi
jijini Dar es Salaam na kukutana na mziki huu mnene na wakutatanisha
uliozikutanisha gari mbili,ukiangaliwa kwa makini utabaini kuwa hili
gari kubwa lenye nambari za Usajili T 544 CKG mali ya Kampuni ya Azania
lilikuwa lipo kwenye njia yake halali kabisa kuelekea Buguruni na huyo
mwenye Gari ndogo lenye nambari za Usajili T806 AVT anaonekana akielekea
Ubungo lakini katika njia ambayo haimruhusu yeye kupita.Kilichotokea hapo
ndio kama inavyoonekana pichani.Sasa sijui huyo mwenye hiyo gari ndogo
alijiona anaendesha Boda boda....!!! Maana hapo alipotaka kupita hata
hapaelezeki.
Hapa hata sijui walitaka kupishana vipi??
Huu mwengine ni wazimu ulioongezewa bangi.
ReplyDeleteMtu kama huyu ni wa kunyang'anywa leseni angalau kwa mwaka mmoja ili ajirekebishe.
Hapa Tanzania ninaweza kupata leseni kwa muda wa masaa mawili. Na ninaweza kukutafutia leseni halali hata kama hujui kuendesha. Wewe tayarisha tu fungu la kutosha. Hii ni Bongoland. Ndivyo tunavyokula hapa. Mambo ya kunyanganywa leseni ni ya huko nchi za nje. Hapa hakuna system. Wewe unaona kashfa za mabilioni kwa wakubwa, unadhani sisi wadogo tunaishije. Mimi ninawaomba mlio nje mrudi mje mtusaidie kurekebisha system hapa. Vinginevyo hapa tunaishi kwa sheria za porini. Survival of the fitest.
ReplyDelete