
Wakati alipozaliwa mtoto huyo, wafanyakazi wa hospitali waliweka
alama ya kuuliza penye kisanduku cha jinsia kwenye fomu ya uzazi mwaka 2009
baada ya kushindwa kuamua kama ni wa kike ama wa kiume.
Wakili wa mtoto huyo ameeleza kufurahishwa na hukumu hiyo
akisema ni hatua moja kwenda mbele katika kutambua watu wenye jinsia mbili
wanaojulikana kitaalamu kama "Intersex persons".
Hukumu hiyo inamaanisha
kwamba sasa mtoto huyo atapatiwa cheti cha kuzaliwa kitachomuwezesha kufaidi
haki zake zote za msingi kama vile elimu, kupata kitambulisho cha Taifa na
kupiga kura. "Sasa watampatia mtoto huyu cheti cha kuzaliwa", alisema
wakili wake Bw. John Chigiti. "Huu ni ushindi..."
Watu
wenye jinsia mbili wamekuwa wakinyanyapaliwa maana hali hiyo haieleweki, ambapo
wengi huiita ni "Mkosi".Mahakama
hiyo pia ilimuamuru Mwanasheria Mkuu kuunda chombo kitakachokuwa na jukumu la
kufanya sensa ya watu wenye jinsia mbili na kutengeneza kanuni na sera kwa
ajili ya kutambulika kwao na usaidizi."Hakika
uamuzi huo unatia moyo sana kwa sababu kama kanuni zinatengenezwa hii ina maana
kuwa watu wa aina hii watatambulika rasmi". alisema Wakili Chigiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...