Salam kwako Ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii,
Tunawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kutujuza mambo mbali mbali yanayoendelea hapa nchini na nje ya mipaka ya nchi yetu,tunawapa BIGI APU sana kwa kweli.
Kupitia libeneke la Globu ya Jamii,naomba nifikishie kero yangu hii kwa wahusika wa Halmashauri ya Jiji,maana leo nilifika pale kwenye stendi kuu ya mabasi (Ubungo Bus Terminal) na kukutana na utaratibu wa kulipisha kiasi cha sh. 300 ikiwa ni gharama ya maegesho ya magari ndani ya stendi hiyo,hali ambayo haiendani kabisa na malipo yanayolipishwa getini pale.
Kiukweli pale haki haitendeki kabisa maana hakuna huduma yeyote ya maana ndani ya Stendi ile kwa hivi sasa,hasa baada ya kituo kicho kuvunjwa vunjwa na hayo maegesho yenyewe tunayolipia hata hayapo na pia bado kuna utaratibu wa kuwalipisha kiasi cha sh. 200 kila mtembea kwa miguu anayeingia kwenye stendi hiyo.
Naomba wahusika wa Halmashauri ya Jiji hasa Manispaa ya Kinondoni kuliangalia swala hili kwa jicho la pili,maana hicho kiasi kinaonekana ni kidogo lakini ni kikubwa sana.
Mdau Mzalendo wa Jijini Dar.
Mie nafikiri hii ni skandal nyingine je wanalipa TRA kiasi gani tunataka kujua.Watanzania sasa hivi tuwe na kila sababu ya kuhoji vitu kama hivi na tummunge mkono mwenzetu aliyetaka kujua. Tegeta Escrow yamefika hapa yalipo kwa sababu ya sisi wananchi kutokutaka kujua mambo yanavyokwenda. Tuache tabia ya woga tukiwa wengi tunao hoji na viongozi wataogopa kufanya haya ya AIBU wanayofanya TUAMKE jamani.
ReplyDeleteMdau Anon wa kwanza baada ya mkerwa....nakubaliana na wewe. Mambo ya kunyamaza ndiyo yana sababisha baadhi ya matatizo serikalini. Kweli ni uwito wa KILA mlipa kodi kuwa makini wa mambo kama haya hasa pale tu yanapozuka. Si kungoja hadi ina halalishwa. Kweli wakati wa kutoa hoja na malalamiko ni sasa dakika hii na si baadae wala si wakati ujao.
ReplyDeleteTatizo wengi watanzania shule hakuna na walio wengi hata hawajui khaki zao,
ReplyDelete