Kampuni
Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao
yake makuu jijini Arusha imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi
katika vituo lenye jina "Kampeni ya USHINDI"linalowashirikisha wadau
mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi
wa kituo hicho Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa
ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha
sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo
alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale
wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi
watajiskia vizuri
Meneja
masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote
walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo
kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis
bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World
garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...