




………………………………………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali
imeazimia kuanza kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza
kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
Azma
imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa
Kigoma.
Bibi
Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango
kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa kiwanja hicho.
“Kama
munavyokumbuka Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza
na kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na
kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika
maeneo ya kimkakati ikiwamo Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.
Kwa
mujibu wa Bibi Mwanri, uendelezaji wa Kiwanja hicho utajumuisha ujenzi
wa jengo la abiria pamoja na miundombinu yake (maegesho ya ndege,
maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka) na kurefusha
barabara ya kuruka na kutua ndege.
Akiwasilisha
taarifa ya maendeleo ya uwanja huo, Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja
cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha alisema kuwa mpaka sasa Mamlaka ya
Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini imekamilisha taratibu za kumpata
mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa usalama na eneo la maegesho ya
ndege.
“Kwa
sasa tunaendelea na kazi ya utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa
ajili ya kazi za ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya
magari, na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa maegesho ya ndege
pamoja na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege,” alisema.
Mhandisi
Neema aliongeza kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpata Mhandisi Mshauri
wa kufanya usanifu wa jengo la abiria uwanjani hapo.
Naye
Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende alisema
kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Mamlaka ya
Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini kwa kushirikiana na Mkoa wa Kigoma
vimeainisha na kufanyia tathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya kazi
hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...