MAKAMPUNI
saba yamethibitisha ushiriki wao katika tuzo za bodi yenye uongozi bora
katika sekta ya kibenki na bima zijulikanazo kama Best Board Leadership
Awards (BBLA), zilizopangwa kufanyika Januari 30, mwakani katika Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mratibu wa tuzo hizo, Bi.
Neema Gerald, imezitaja benki zilizothibitisha kushiriki katika tuzo
hizo kuwa ni pamoja na Benki ya Posta (TPB), Benki ya Exim na Benki ya
CRDB.
Aliyataja
makampuni ya bima yaliyothibitisha kushiriki katika tuzo hizo kuwa ni
Heritage Insurance, Alliance Insurance Corporation, Alliance Life
Assurance na Strategis Insurance (T) Limited.
Tuzo hizo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wakurugenzi katika Sekta ya Kibenki na Bima.
Bi.
Neema aliendelea kuzisihi kampuni zaidi zilizopo katika sekta ya
kibenki na bima kujitokeza kwa wingi ili kujisajili katika tuzo hizo
zilizoandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na
Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa makampuni yaliyoonyesha mwamko wa
kushiriki kwenye tuzo hizi katika hatua hizi za mwanzo za maandalizi,”
alisema na kuongeza:
“Tuzo
hizi zitatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia
taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo
walilobobea kiutalaam. Hivyo ningependa kuziasa kampuni zaidi kujitokeza
na kushiriki,” alisema Bi. Neema.
Alibainisha
kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na
jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.
Tathmini
hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala
la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya
taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na utendaji wake.
Alitaja
maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa
mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji
watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha
utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.
Bi.
Neema aliwataja wadhamini wa tukio hilo la kipekee kuwa ni pamoja na
Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax
Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media.
"Tumeona
umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa
bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi
ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa,
sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakua nazo zinapaswa
kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.
Bi.
Neema alisema kuwa ni utamaduni uliozoeleka kwa Maafisa Watendaji Wakuu
na Wakurugenzi Wakuu pekee kuthaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au
jamii nzima kwa ujumla.
"Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema.
Bi.
Neema aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini
kipindi ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa
huku makampuni mengi zaidi ya bima yakijitokeza na masoko zaidi
kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.
"Kwa
mabadiliko haya yanayotokea wakati huu, hasa katika sekta ya fedha
ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na benki yamekuwa yakifungua
biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya
bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...